Sunday, 19 June 2016

Waziri Cameron aonya juu ya Uingereza kujitoa EU

Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron ameonya leo hii juu ya kutokuwepo kwa fursa nyingine ya kurudi katika Umoja wa Ulaya iwapo nchi hiyo itaamuwa kujitowa katika umoja huo wakati wa kura ya maoni.

David Cameron kiongozi wa serikali ya kihafidhina nchini Uingereza ameliambia gazeti la "Sunday Times"  kwamba hakutakuwepo na uwezekano kwa nchi yake kurudi tena katika Umoja wa Ulaya iwapo hapo Alhamis wananchi wengi wataamuwa kujitowa katika umoja huo.

Onyo hilo ambalo amelitoa kupitia gazeti la "Sunday Telegraph" linaonekana kama kampeni kuhamia katika vyombo vya habari kutokana na kusitishwa kwa mikutano mikubwa ya hadhara baada ya kuuwawa kwa mbunge wa chama cha Labour Jo Cox siku ya Alhamis.

Meya wa zamani wa jiji la London Boris Johnson, mtu muhimu katika harakati za kutaka Uingereza ijitowe Umojawa Ulaya ameyagaukia magazeti mashuhuri ya Jumapili kushinikiza hoja zake. Bunge la Uingereza limeitisha kikao maalum kesho cha kumbukumbu kwa heshima ya Cox.

No comments:

Post a Comment