Saturday, 18 June 2016
Wazazi wenye mfumo dume kukiona Nyamagana
Baraza la Watoto Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, limeiomba jamii kufichua wazazi wanaoendeleza mila na desturi zinazokandamiza haki zao, ikiwamo ukeketaji wa mabinti.
Akihutubia wazazi na watoto katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika Shule ya Msingi Mabatini juzi, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Baraka Konisaga amesema vitendo vingi vya ukatili na unyanyasaji dhidi ya watoto hufanyika ndani ya jamii, lakini havifichuliwi hadi madhara yanapokuwa makubwa.
Konisaga amesema iwapo kila mmoja atatimiza wajibu kwa kupinga, kukemea na kufichua vitendo vya unyanyasaji dhidi ya watoto, Taifa litafanikiwa kutekeleza kwa vitendo kaulimbiu ya mwaka huu isemayo: “Ubakaji na ulawiti kwa watoto vinaepukika, chukua hatua kumlinda mtoto.”
Labels:
Habari za Kijamii
Location:
Mwanza, Tanzania
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment