Saturday, 18 June 2016
Mahakama Kuu kanda ya Mwanza kuamua ya Polisi na CHADEMA
Uamuzi wa kesi iliyofunguliwa na Chadema dhidi ya Polisi kupinga amri ya kupiga marufuku maandamano na mikutano ya kisiasa utatolewa Juni 21 na Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza.
Jaji Mohamed Gwae anayesikiliza shauri hilo, alifikia uamuzi huo baada ya kusikiliza hoja za mawakili wa pande zote za utetezi na mleta maombi.
Awali, Mawakili wa utetezi, Robert Kidando na Obadia Kajungu waliomba Mahakama kutupilia mbali maombi ya Chadema kuruhusiwa kufungua kesi yaliyowasilishwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, kwa madai kuwa hayajakidhi mahitaji ya kisheria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment