Polisi nchini Ubelgiji imewafungulia mashitaka watu watatu kwa tuhuma za kupanga mashambulizi mapya ya kigaidi nchini humo mwishoni mwa wiki hii.
Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa watu hao waliotiwa mbaroni walikuwa wanapanga kufanya mashambulizi mjini Brusssels wakati wa moja ya mchezo wa timu ya taifa ya Ubeligiji inayoshiriki mashindano ya kuwania kombe la mataifa barani Ulaya-EURO 2016.
Polisi nchini humo waliendesha msako katika nyumba na gereji kadhaa usiku kucha hapo jana na kufanikiwa kuwatia mbaroni watu 12. Washukiwa tisa wa mipango ya shambulizi hilo waliachiwa baadaye.
Waziri Mkuu, Charles Michel amesema hali imedhibitiwa ingawa usalama wa nchi hiyo uko katika uangalifu mkubwa. Ubeligiji inaendelea kubakia katika hali ya tahadhari kubwa dhidi ya ugaidi kutokana na mashambulizi ya mjini Brussels Marchi 22 mwaka huu ambapo watu 32 waliuawa.
No comments:
Post a Comment