Waziri wa mambo ya Kigeni wa Luxembourg Jean Asselborn amesema kujitowa kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya kunaweza kusababisha kuchukuliwa hatua kama hiyo na mataifa mengine wanachama katika eneo la Ulaya Mashariki.
Waziri Asselborn amenukuliwa alipozungumza na toleo la gazeti la leo Jumapili la hapa Ujerumani "Tagesspiegel am Sonntag". Amesema lilikuwa kosa la kihistoria kwa Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameroon hata kufikiria juu ya kuitisha kura ya maoni, kuhusu uanachama wa Uingereza katika Umoja wa Ulaya.
Aidha ameongeza kuwa hata kama Uingereza itaamua kuendelea kusalia katika Umoja wa Ulaya katika kura ya maoni iliyopangwa kufanyika Juni 23, hakutaondosha tatizo lililosababisha mtazamo hasi wa Waingereza dhidi ya Umoja wa Ulaya.
No comments:
Post a Comment