Saturday, 18 June 2016
Wahamiaji 19 wafa baada ya kukosa hewa huko Kongo
Walinzi katika mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Zambia wameipata miili ya wahamiaji 19 wa Ethiopia waliokufa kutokana na ukosefu wa hewa katika lori lililokuwa limebeba karibu wahamiaji 100.
Maafisa wanasema walishutushwa na harufu kali ya kuchafuwa kutoka katika lori lenye namba za usajili za Zambia, ambapo wengine 76 wamekutwa bado wako hai.
Mkuu wa kikosi cha walinzi wa mpakani Jean-Pierre Lubosha amesema kwamba "walisimamisha lori hilo kutokana na harufu kali iliyokuwepo".
Manusura wote wamekiri kwamba wamekimbia nchi yao wakielekea Afrika ya Kusini kupitia Kenya, wakitafuta maisha bora. Madereva wa gari hilo walidai walikuwa wakisafirisha samaki wadogo. Miili na walionusurika wamekabidhiwa mamlaka ya Zambia.
Mamlaka za Zambia zimesema uchunguzi utafanyika kubaini watu walio katika mtandao wa biashara haramu ya kusafirisha binadamu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment