Saturday, 18 June 2016

Steinmeier aionya NATO

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier amesema mazoezi ya kijeshi ya hivi karibuni ya jumuiya ya kujihami ya NATO, yanaweza kuvuruga hali ya kiusalama Mashariki mwa Ulaya. Ametoa wito wa mazungumzo na Urusi kabla ya mkutano wa jumuiya hiyo hapo Julai mjini Warsaw. Katika matamshi yake yaliyochapishwa hii leo katika gazeti la Ujerumani la Bild am Sonntag, Steinmeier amekosoa luteka kijeshi ya hivi karibuni ya NATO mashariki mwa Ulaya kwa kusema kuwa haina tija kwa usalama katika ukanda huo. Juni 7 mwaka huu, NATO ilianzisha luteka ya kijeshi iliyoyaita "Anakonda 16" ambayo ilimithilisha shambulio la Urusi kwa Poland. Mazoezi hayo ya kijeshi yaliyochukua wiki mbili yalihusisha vikosi 31,000, vikiwemo 14,000 kutoka Marekani, 12,000 kutoka Poland na 1000 kutoka Uingereza halikadhalika ndege za kivita, meli pamoja na magari 3000 ya kijeshi.

No comments:

Post a Comment