Wednesday, 22 June 2016

Ujerumani yashutumiwa na UNICEF kuhusu watoto wakimbizi

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwashughulikia Watoto UNICEF, limechapisha ripoti jana inayokosoa mazingira wanayoishi watoto wakimbizi nchini Ujerumani.

UNICEF imesema watoto wakimbizi wana viwango vya chini kabisa vya usalama, huduma za matibabu na elimu kuliko wenzao waliozaliwa Ujerumani. Pia ripoti hiyo imesema watoto wakimbizi wanashughulikiwa tofauti kabisa kwa kutegemea uwezekano wa wao kuruhusiwa kuishi Ujerumani.

Shirika hilo la Umoja wa Mataifa limesema hali hiyo inasababisha tatizo la muingiliano wa watoto katika jamii wakati wanapoanza masomo nchini Ujerumani. Ujerumani ni nchi inayoongoza kwa kuwakaribisha wahamiaji na wakimbizi wanaowasili barani Ulaya kutoka katika mataifa mbalimbali yenye migogoro.

No comments:

Post a Comment