Wednesday, 22 June 2016

Tembo auawa kwa umeme Uganda


Ndovu mmoja katika mbuga ya wanyama pori ya Queen Elizabeth nchini Uganda, amekufa baada ya kupigwa na umeme, kwa mujibu wa gazeti la nchi hiyo la Daily Monitor.

Shirika la wanyamapori nchini humo (UWA) linasema kuwa mzoga wa ndovu huyo, ulipatikana asubuhi kwenye nyaya za umeme zinazounganisha umeme na transfoma moja.

Ukuta wa nyaya uliokuwa ukizungusha transfoma hiyo, ulikuwa umeharibiwa wakati ndovu huyo alipokuwa akiharibu kuuvuka na kujiokoa.

No comments:

Post a Comment