Friday, 17 June 2016
TASAF kunufaisha vijiji 54 Karagwe
Mratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe, Edius Rwangoga amesema kati ya vijiji 71 vya wilaya hiyo ni vijiji 54 pekee vilivyokidhi vigezo vya kupokea fedha za mfuko huo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zaidi ya Sh3.2 milioni kwa kaya 9,534 za wilaya hiyo juzi, amesema kaya 9, 534 pekee kutoka wilaya hiyo ndizo zitakazonufaika.
“Vijiji 54 kati ya 71 ndivyo vitanufaika na mpango wa kunusuru kaya maskini kwa awamu ya sita inayoanza kutekelezwa kuanzia mwezi huu,” amesema Rwangoga.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Wilaya hiyo, Ashura Kajuna amewataka walengwa kuweka malengo ya kuzitumia na kupata mabadiliko ya maisha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment