Saturday, 18 June 2016
Nyati waua Mkoani Manyara
Mkazi wa Mererani mkoani Manyara Samson Samson (32), amefariki dunia baada ya kushambuliwa na Nyati (Mbogo) wilayani Karatu katika mashamba ya kahawa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amesema jana kuwa tukio hilo limetokea juzi saa kumi jioni wakati Samson alipokuwa akipita katika mashamba hayo.
“Mtu huyo ameuawa na Nyati alipokuwa akitoka kusalimia ndugu zake Karatu. Mwili wake umekutwa kwenye mashamba hayo ukiwa na majeraha ya kutobolewa na mnyama huyo huku kundi lingine la wanyama hao likiwa limemzunguka, ” amesema Mkumbo.
Kamanda Mkumbo amesema kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Lutheran.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment