Saturday, 18 June 2016

Iran yaipongeza Iraq baada ya Mji wa Fallujah kutwaliwa na Wanajeshi wa Serikali


Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif ameipongeza serikali na watu wa Iraq kufuatia kukombolewa mji wa kati wa Fallujah kutoka kwa magaidi wa kundi la wakufurishaji wa ISIS au Daesh.

Katika ujumbe kwa waziri mwenzake wa Iraq Ibrahim al Jaafari, Zarif ameutaja ushindi wa Fallujah kuwa ni dhihirisho la ushindi kwa wale wanaopigana kwa njia ya Mwenyezi Mungu.

Zarif pia ameelezea matumaini yake kuwa jeshi la Iraq litapata ushindi zaidi katika vita vyake dhidi ya magaidi wakufurishaji wa ISIS huku akisisitiza umuhimu wa kulindwa umoja wa kitaifa nchini humo.

Haider al-Abadi, Waziri Mkuu wa Iraq pia amepongeza hatua ya kukombolewa kikamilifu mji wa kistratejia wa Fallujah toka mikononi mwa ISIS na kusema kuwa kundi hilo la kigaidi na kitakfiri halina nafasi katika nchi hiyo ya Kiarabu.

Akilihutubia taifa jana kupitia runinga ya dola, al-Abadi amesema kuwa kundi la Daesh halina nafasi katika taifa hilo na kwamba wanachama wake watazidi kushindwa na kusambaratishwa kwa kuwa wananchi wote wameungana dhidi yao.

No comments:

Post a Comment