Bahrain imemvua uraia wake mhubiri mmoja mashuhuri wa Kishia baada ya kumtuhumu kwa kueneza migogoro inayohusishwa na dini na vurugu.
Mhubiri huyo, Isa Qassim, mwenye umri wa miaka 79, anazingatiwa kuwa kiongozi wa kiroho wa Waislamu wa Kishia walio wengi.
Bahrain, hata hivyo, inaongozwa na utawala ulio na Wasunni wengi. Mamia ya watu waliripotiwa kukusanyika nje ya nyumba ya Qassim kulalamika kuhusu uamuzi wa kumpokonya uraia wake.
Msemaji wa Ikulu ya Rais nchini Marekani John Kirby pia aliikosoa hatua hiyo akisema Marekani haifahamu kuhusu ushahidi wowote wa msingi unaohalalisha hatua hiyo na kuwa Qassim haonekani kuwa alipewa fursa yoyote ya kuhoji tuhuma dhidi yake kabla ya uamuzi kutolewa na serikali.
Bahrain ni mshirika mkuu wa Marekani na pia Marekani ina kambi ya jeshi lake la wanamaji nchini humo.
No comments:
Post a Comment