Wednesday, 22 June 2016

Mh. Mwalimu ataka maelezo toka kwa MNH


Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameutaka uongozi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kutoa maelezo kwa kina juu ya taarifa za uamuzi wa kuwataka wagonjwa wachangie huduma za matibabu, zikiwamo dawa za kufubaza makali ya Ukimwi na Kifua Kikuu.

Amesema baada ya kupata maelezo hayo, wizara itatoa taarifa rasmi.
Kabla ya agizo la Waziri Mwalimu, Naibu wake, Dk Hamis Kigwangalla akizungumza bungeni, Serikali haijabadilisha chochote katika Sera ya Afya, watu waliorodheshwa kupata matibabu bure kama wazee, watoto chini ya miaka mitano na wajawazito wasipate hofu. “Hakuna dawa zozote za HIV zitakazouzwa wala za kifua kikuu,” alisema.

No comments:

Post a Comment