Wednesday, 22 June 2016
Dr. Tulia awachoka UKAWA
Naibu Spika, Dk Tulia Ackson leo ameonekana kuchoka kitendo cha wabunge wa Ukawa kususia vikao vyake na kuwataka watoke haraka bungeni kama hawahitaji kuendelea na kikao.
Dk Tulia amesema hayo wakati wabunge hao walipoanza kutoka bungeni baada ya dua.
Amewataka watoke haraka kwa sababu walikuwa wanachelewesha shughuli za Bunge.
Leo ni siku ya 19 wabunge hao wanasusia vikao hivyo vinavyoendeshwa na Dk Tulia, juzi walitangaza kuvunja uhusiano wa kawaida na wabunge wa CCM jambo ambalo limelaaniwa na wawakilishi hao wa chama tawala.
Labels:
Habari za Kisiasa
Location:
Dodoma, Tanzania
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment