Thursday, 16 June 2016
CRDB yamwaga zawadi kwa akina Mama waliojifungua tarehe ya Siku ya mtoto Afrika
KATIKA kusherekea siku ya mtoto wa Africa, Benki ya CRDB Tawi la Mlimani City limetoa zawadi mbalimbali kwa watoto na kimama waliojifungua siku ya leo.
Zawadi hizo zilizolenga kutambua mchango wa watoto wa kiafrica ambao ndio wajenzi wa taifa pamoja na wateja wa baadae wa taasisi za kibenki.
“Katika kusherekea siku hii adhimu na muhimu, Benki ya CRDB kupitia tawi lake la Mlimani City tumekuja kutoa zawadi kwa mama zetu hawa maana huwezi kusherekea siku ya mtoto bila kumpongeza na mama pia pamoja na kuwatakia kila la kheri wale ambao wanatarajia kujifungua,” alisema Mkurugenzi wa tawi hilo, Allen Kilango.
Zawadi hizo zenye thamani ya shillingi million 3.2 zilitolewa katika hospitali ya Sinza Palestina. Tawi hilo lilitoa sukari, maji, sabuni za kufulia, majani ya chai, Pampas pamoja na vifaa vingine kwa ajili ya kuwatunza watoto wachanga.
Akitoa shukrani kwa niaba ya wazazi wengine waliopo wodini, Tunu Tebesi amesema wanashkuru sana kwa msaada huo na umewapa moyo sana kama wamama na pia kuwasaidia watoto wao maana wengine walikuwa hawana uwezo wa kununua baadhi ya vitu walivyopewa.Katika siku hiyo ya mtoto wa Africa leo, jumla ya watoto 45 walizaliwa katika hospitali hiyo jana, wakiume wakiwa 15 na wakike 30.
Labels:
Habari za Kijamii
Location:
Dar es Salaam, Tanzania
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment