Saturday, 18 June 2016

CHADEMA: Tunataka Demokrasia


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani Kilimanjaro kimeiomba Serikali ya Rais John Magufuli iache kuminya demokrasia na badala yake ifanye kazi yake.

Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Philemon Ndesamburo amesema jana kuwa  tamko la Jeshi la Polisi kuzuia mikutano ya siasa ya hadhara kwa nchi nzima limezua maswali mengi kwa wananchi yasiyo na majibu.

“Siku chache zilizopita nilipokea taarifa kuwa makada wetu wanaovaa sare za chama wakiwa katika mizunguko ya kawaida mitaani wakikutana na polisi wanawatisha kisa wamevaa sare hizo,” amedai Ndesamburo.

No comments:

Post a Comment