Showing posts with label Amani. Show all posts
Showing posts with label Amani. Show all posts

Saturday, 2 July 2016

Kundi la Taliban lataka uhusiano kati ya Afghanistan na Marekani ufe


Kiongozi wa kundi la wapiganaji la Taliban, Maulawi Haibatullah Akhundzada, hii leo amezungumza kwa mara ya kwanza tangu kuchaguliwa kwake mwezi mei, ambapo ameitaka Marekani kuondoka Afghanistan.

Maulawi Haibatullah Akhundzada amesema uwepo wa Marekani na washirika wake nchini Afghanistan hautaathiri juhudi za makundi ya kijihadi.

Amesema kuwa Taliban haitaki kuwa na ukiritimba wa mamlaka, japo akasisitiza kwamba ni lazima serikali ya Afghanistan ikatize uhusiano wake na Marekani, kama hatua ya kwanza ya mchakato wa amani katika misingi ya sheria za kiislamu.

Israel yaishambulia Gaza


Ndege za kivita za Israeli zimetekeleza msururu wa mashambulzi ya asubuhi mapema huko Gaza.

Jeshi la Israeli linasema limeshambulia maeneo manne yanayohusishwa na wapiganaji wa Hamas ambao wanadhibiti eneo hilo.

Kulingana na taarifa kutoka kwa vyanzo nchini Palestina, watu wawili wameuawa.

Awali kombora lililofytuliwa kutoka Gaza liligonga jengo la shule ya chekechea japo halikuwa na watu.