Monday, 4 July 2016

Wizara ya Afya yampongeza RC Makonda


Wizara ya Afya imempongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kupiga marufuku matumizi ya shisha na uvutaji sigara hadharani kama hatua ya kupunguza madhara ya tumbaku na dawa za kulevya katika jamii.

 Mbali na pongezi hizo, wizara hiyo imerejea na kusisitiza agizo lake la Machi 12, 2015 la kuzuia matumizi ya sigara na matumizi ya bidhaa za tumbaku katika maeneo ya umma.

Taarifa iliyotolewa leo na kitengo cha habari cha wizara hiyo, imesema uchunguzi wa kitalaam uliofanyika umebaini kuwa shisha ina madhara kwa afya ya watumiaji hasa vijana na watoto.

“Watumiaji wa shisha wanatumia kiwango kikubwa cha tumbaku kwa muda mfupi, hali inayoongeza madhara yatokanayo na tumbaku kama saratani, magonjwa ya mapafu, kibofu cha mkojo, tezi dume, koo, mdomo na kiywa, ngozi, ini na ubongo,” imesema taarifa hiyo.

Pia imebainika kwamba matumizi ya shisha huambatana na kuongezewa dawa nyingine za kulevya na hivyo hufanya watumiaji wa wa kilevi hicho kupata uraibu wa dawa za kulevya., hivyo kufanya matumizi ya dawa hizo kuwa kosa la jinai.

No comments:

Post a Comment