Friday, 1 July 2016
Daktari: Watu wenye Kisukari na Shinikizo la damu wapewe kipaumbele
Daktari kutoka Taasisi ya Afya Ifakara, Herry Mapesi ameshauri wagonjwa wenye matatizo ya kisukari na shinikizo la damu waangaliwe kwa ukaribu na kupatiwa huduma za dawa kama walivyo wagonjwa wenye maambukizi ya Ukimwi.
Alitoa ushauri huo jana jijini Dar es Salaam kwenye mkutano ulioandaliwa na taasisi hiyo kwa lengo la kuongeza ufahamu katika eneo la afya.
Alisema kwa sasa wagonjwa wa Ukimwi wanaopata dawa mapema huishi maisha marefu sawa na ambao hawana maambukizi, inabidi nguvu pia ielekezwe kwenye magonjwa hayo kwa kuwa yamekuwa yakisababisha vifo vingi.
Alisema Ukimwi umeonekana kuwa ni ugonjwa wa kawaida kwa kuwa tangu dawa zilipopatikana kwenye mwaka 2005, utafiti unaonesha wagonjwa hao wanaishi sawasawa na wasio na maambukizi, endapo wataanza dawa mapema na kuzinywa vizuri kinga zao zitapanda.
Labels:
Afya ya Jamii
Location:
Dar es Salaam, Tanzania
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment