Friday, 1 July 2016
Uzazi: Mama ruksa kutumia mayai ya bintiye kupata mjukuu
Mwanamke ambaye anataka kutumia mayai ya uzazi ya binti yake ili kumzaa mjukuu wake ameshinda kesi mahakanani na kuruhusiwa kufanya hivyo.
Mwanamke huyo wa umri wa miaka 60 alikuwa amekatazwa kupeleka mayai ya binti yake kwenye kliniki moja nchini Marekani hali iliyosababisha akate rufaa.
Binti yake ambaye aliaga dunia mwaka 2011, anaripotiwa kumuambia mama yake amzalie watoto wake. Lakini mama huyo alishindwa katika kesi mwaka uliopita.
Hata hiyo aliruhusiwa kupinga hukumu hiyo katika mahakama ya rufaa mjini London mbele ya jopo la majaji watatu.
Mwaka 2014 halmashauri inayohusika na mayai ya uzazi, ilisema kuwa mayai hayo hayangetolewa mjini London, kwa sababu binti wa mama huyo (marehemu) hakuwa ametoa idhini kamili kabla ya kifo chake akiwa na umri wa miaka 28.
Lakini kwenye kesi ya sasa mawakili waliwaambia majaji kuwa, mwanamke huyo alikuwa anataka kutimiza matakwa ya binti yake ya kuzaa mtoto akitumia mayai yake na kisha amlee mtoto huyo.
Labels:
Haki na Sheria
Location:
London, Uingereza
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment