Monday, 4 July 2016
Mtandao wa Facebook wasaidia katika kubaini wahusika wa Uvamizi Bangladesh
Maafisa wa usalama nchini Bangladeshi wametumia mtandao wa kijamii wa Facebook kuwatambua watatu kati ya magaidi 6 walioshambulia mji mkuu wa Dhaka.
Polisi wanaochunguza shambulizi hilo baya zaidi la kigaidi kuwahi kutokea nchini humo wanasema Facebook imewasaidia sana.
Afisa hao wa polisi wametangaza hayo huku nchi hiyo ikianza siku mbili za maombolezo.
Ingawa kundi la wapiganaji la Islamic State lilisema lilihusika kutekeleza shambulio hilo, ambalo lilimalizika baada ya makamando walipovamia jengo la mkahawa jana asubuhi.
Waziri mmoja amesema watu hao walikuwa kwenye kundi la Mujahdeen Bangladesh wala sio Islamic State.
Watu 20 waliuawa, wengi wao wageni, pamoja na askari polisi wawili.
Wakuu wanasema washambuliaji wote walikuwa wa Bangladesh, na walikuwa wakisakwa na maafisa wa usalama. Tayari wapiganaji sita waliuwawa na mmoja alikamatwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment