Tuesday, 5 July 2016
Mameya wa zamani Rwanda kufungwa maisha Jela
Wakili Mkuu wa Serikali ameomba Jumatatu hii kifungo cha maisha jela dhidi ya mameya wawili wa zamani wa Rwanda, wanaotuhumiwa kushiriki katika mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi katika kijiji chao mashariki mwa Rwanda mwezi Aprili, 1994.
Baada ya miezi miwili kesi hiyo ikisikilzwa mbele ya Mahakama ya Paris, Philippe Courroye amewataja Octavien Ngenzi, mwenye umri wa miaka 58, na Tito Barahira, mwenye umri wa miaka 65, kama wahusika muhimu katika mauaji ya kimbari yaliyotokea katika wilaya yao ya Kabarondo, akimtaja Octavien Ngenzi kama "kiongozi" na tito Barahira kama mfadhili wa mapanga.
Watu hao wawili, ambao wote wanakataa kushiriki kwao katika mauaji ya kimbari, wamesikiliza hukumu dhidi yao huku wakipokea hukumu hiyo kwa shingo upande: Ngenzi "Yuda" ambaye hakufanya chochote kwa "kuzuia mauaji hayo" lakini "aliyasimamia". Barahira "mtekelezaji", ambaye alikua"akitoa maelekezo" na kushirikiana na wauaji, huku akibebelea mkuki mkononi.
"Wote hao walikua wauaji na wandaaji wa mauaji ya kimbari", wao, wanakabiliwa na mashtaka, "kukosa kukiri kosa lao, pamoja na kuomba msamaha" kwa kukana kosa lao hadi dakika ya mwisho.
Philippe Courroye amekumbusha kwamba watu hawa, waliokamatwa nchini Ufaransa wamehukumiwa chini ya uwezo wa mamlaka nzima ya mahakama za Ufaransa. Kesi hii ni ya pili kushughulikiwa nchini Ufaransa kuhusu mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment