Monday, 4 July 2016
CHADEMA waishutumu vikali Polisi
Katibu wa Chadema, Mkoa wa Morogoro Samuel Kitwike amesema wanalaani vitendo vya ukiukwaji wa Katiba ya nchi vinavyofanywa na vyombo vya dola kwa makusudi kwa lengo la kudhoofisha demokrasia nchini.
Kauli hiyo inafuatia Umoja wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Wanachama wa Chadema (Chaso) kuzuiwa kufanya mahafali.
Awali, chama hicho mkoani hapa kilieleza kuchoshwa na vitendo vya ukandamizaji vinavyodaiwa kufanywa na polisi.
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei amesema polisi wana wajibu wa kuhakikisha raia wanakuwa salama.
Labels:
Haki na Sheria
Location:
Morogoro, Tanzania
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment