Saturday, 18 June 2016

Zanzibar kuboresha kanuni za Soka la vijana


KAMATI ya Soka ya Vijana Taifa Zanzibar leo inatarajia kukutana na Makatibu na Wenyeviti wa Kamati za Soka la vijana wilaya za Unguja.

Akizungumza na gazeti hili, Katibu wa Kamati hiyo, Abdallah Thabit, alisema kikao kingine kama hicho kitafanyika pia katika wilaya za Pemba.

Alisema lengo kuu la kukutana huko ni kuzifanyia marekebisho kanuni zao wanazozitumia katika mashindano ya vijana.

Alisema wameamua kuzifayia marekebisho kanuni hizo za kuendesha mashindano baada ya kuona kwamba ni miaka mingi hawajazifanyia marekebisho.

“Nafikiri ni miaka mingi sasa kanuni zetu hatujazifanyia marekebisho, nakumbuka kwa mara ya mwisho tulifanya marekebisho mwaka 2010,” alisema.

Pia alisema kuwa kupitia kikao hicho watapanga kwenda kuzungumza na Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) kuhusiana na suala la kuanza kwa usajili na uhamisho wa wachezaji.

Alisema hatua hiyo itasaidia ili wachezaji wote ambao wanatoka katika madaraja ya vijana basi fomu zao za uhamisho zitoke katika madaraja yao ya vijana.

Kutokana na hilo, alisema kamati itaandaa fomu maalumu ili kamati zao zipate fedha ambazo ni haki zao tofauti na sasa ambapo wachezaji wote wanapohamishwa hutumia fomu kutoka wilaya.

No comments:

Post a Comment