Saturday, 18 June 2016

Washukiwa 12 wa shambulizi wakamatwa Mjini Brussels

Watu12 wanaoshukiwa kupanga mashambulizi mapya wamekamatwa nchini Ubelgiji usiku wa kuamkia leo, baada ya polisi kufanya msako katika nyumba zipato 40 nchini humo. Taarifa ya ofisi ya mwendesha mashitaka mkuu imesema leo hii kwamba kuhusiana na uchunguzi kuhusu ugaidi, watu 40 wamehojiwa na12 kati ya hao wamekamatwa. Jaji anayesimamia uchunguzi huo ataamuwa uwezekano wa kuendelea kushikiliwa kwa watu hao. Ulaya ipo katika hali ya tahadhari kubwa kutokana na michuano ya ubingwa soka barani Ulaya ya euro 2016 yanayoendelea katika nchi jirani ya Ufaransa. Televisheni ya taifa ya VTM imesema watu hao waliokamatwa walikuwa wanapanga shambulizi mjini Brussels mwishoni mwa juma hili wakati wa mchezo wa Ubelgiji katika michuano ya ubingwa wa Ulaya ya euro 2016. Brussels ilishambuliwa mwezi Machi ambapo jumla ya watu 32 walipoteza maisha.

No comments:

Post a Comment