Sunday, 19 June 2016
Waliotafuna fedha za Miradi ya barabara kutiwa nguvuni
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego na Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba, wameagiza kukamatwa kwa watendaji wanaotuhumiwa kwa ubadhirifu wa fedha za ujenzi wa barabara na kufikishwa mahakamani.
Akizungumza katika kikao maalumu cha kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Dendego amesema kutolewa kwa agizo hilo kunatokana na kukiukwa kwa vitu hiyo, kwani tume ya tathmini iliyoundwa kwa ajili ya zabuni ilikuwa na watu wawili kinyume na taratibu na kiasi cha fedha alizoomba mhusika kilibadilishwa kwa kuondolewa kwa nyaraka kwenye dodoso la Serikali na kubadilishwa.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Namkulya Salum, amesema Sheria ya manunuzi ya umma inaeleza kuwa tume ya tathmini iundwe na wajumbe watatu, lakini wasiozidi watano ila iliundwa ya wajumbe wawili kinyume na taratibu za kisheria.
Labels:
Habari za Kisiasa
Location:
Mtwara, Tanzania
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment