Friday, 17 June 2016

Waliokimbia Nigeria wateseka Nigeri


Wanigeria waliokimbia Boko Haram wateseka Niger
Raia kadhaa wa Nigeria ambao ni miongoni mwa maelfu ya watu waliolazimika kuyahama makazi yao wakikimbia mashambulizi yanayofanywa na kundi la itikadi kali la Boko Haram wanaishi katika mazingira ya taabu huku wengi wao wakikosa huduma za chakula na kiafya.  Waziri wa mambo ya ndani wa Niger amethibitisha.  Kundi la itikadi kali la Boko Haram lilishambulia kituo kimoja cha kijeshi cha Bosso katika mkoa wa Diffa nchini Niger mnamo Juni 3 na kuwaua wanajeshi 26 wakiwemo wawili kutoka nchi jirani ya Nigeria. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wakimbizi limesema kiasi ya watu 50,000 hadi sasa wamelazimika kuyahama makazi yao tangu kufanyika kwa shambulizi katika mji wa Bosso nchini Niger ambao uko karibu na mpaka wa Nigeria na Chad.

No comments:

Post a Comment