Friday, 24 June 2016
Tanzia: Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa afariki dunia
Rais wa zamani wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa John Ashe ,ambaye alikuwa akituhumiwa katika kashfa ya rushwa, amefariki dunia kutokana mshtuko wa moyo hapo jana akiwa na umri wa miaka 81.
Maafisa wa serikali ya Marekani walimkamata Ashe ambaye alikuwa rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa mwaka moja tokea mwezi wa Septemba mwaka 2013 kwa madai ya kukubali kupokea hongo ya dola milioni 1.3 kutoka kwa tajiri mkubwa wa Kichina wa biashara za ardhi na majumba.
Pia alifunguliwa mashataka ya kukwepa kulipa kodi katika miezi ya karibuni, alikuwa katika mazungumzo ya kupatiwa msamaha. Kukamtwa kwake kulikuwa pigo kubwa kwa Umoja wa Mataifa ambao uko katika juhudi za kupigania utawala bora usiokuwa na rushwa duniani kote.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment