Monday, 20 June 2016
Senate nchi Matekani kupiga kura ya uuzaji wa silaha
Wiki moja baada ya shambulizi baya katika klabu moja ya mashoga mjini Orlando Florida kutokea , baraza la senate la Mareknai linatarajiwa kupigia kura mapendekezo kadhaa ya kuzuia uuzaji wa bunduki kwa watuhumiwa wa ugaidi na kuongeza ukaguzi kwa watu wanaonunua bunduki hapa Marekani.
Taarifa zinasema kuwa kengele za kanisa zililia huko Orlando wiki moja baada ya Omar Mateen kuanza kufyatuwa risasi katika klabu ya Pulse. Mchana familia zenye kuomboleza , wanazika wapenzi wao.
Seneta wa chama cha Democrat Chris Murphy alisema hawafanyi kitu chochote chochote kile na kwamba amechoshwa na mauwaji ya watu wasio na hatia, na amechoshwa na baraza hili kutokuchukuwa hatua.
Wademokrats waliongoza baraza la senate kwa saa 15 wakidai ipigwe kura dhidi dhidi ya sheria isiyokuwa na nguvu kwa muda mrefu ya kupunguza ghasia za bunduki.
Naye seneta Cory Booker kutoka chama cha Democrat alisema, "Imetosha. Imetosha. Imetosha. Hatuwezi kuendelea hivi na kazi kama kawaida katika baraza hili."
Warepublican wanaemdelea kusisitiza kwamba kulenga kudhibiti bunguki siyo mwongozo mzuri. Wanasema wanahitakji kuwa na mkakati ulio bora ili kuweza kulishinda kundi la ISIS ambalo ndio linashawishi mashambulizi yanayokuwa nchini hapa. Lakini baadae warepublican walikubali upigaji kura ufanyike jumatatu.
Seneta Chris Muphy wa chama cha Democrat alisema, "Tuna nia ya dhati kutoka kwa republican kuwasilisha hatua mbili kwenye baraza la senate kupigiwa kura. Moja ni kuongeza ukaguzi unaofanywa, na pili kuwatowa magaidi katika orodha ya watu wanaoweza kununua bunduki."
Kura pia zinatarajiwa kutoka kwa wareoublican ambazo zinaelezea haki za wamiliki bunduki.
Lakini seneta Mrepublican Pat Toomey anasema hatutaki magaidi kuweza kuingia dukani na kununua bunduki. Na hatutaki raia asiye na hatia anayefuata sharia kunyimwa haki zake kwa mujib wa kipengele cha 2 cha katiba kwa sababu yuko kwa bahati mbaya kwenye orodha pamoja na magaidi.
Hatua ya senate juu ya udhibiti wa bunduki haionekani kuwa itafikiwa muafaka wa karibuni na kadhalika katika bunge.
Naye spika wa bunge kutoka Republican, Paul Ryan, alisema, "Inakwenda baada ya mabadiliko ya kipengele cha pili ni jinsi gani unazuiya ugaidi? La, hio sio njia ya kusitisha ugaidi."
Wiki ilopita huko Orlando, rais alitowa ombi la kuondokana na migawanyiko ya kisiasa.
Rais Obama alisema, "Niliwakumbatia wanafamila wanaoomboleza na wazazi, na wakauliza kwanini hili linaendelea kufanyika. Na wakaomba tufanye Zaidi kuzuia mauwaji. Hawajali kuhusu siasa."
Wademokrat na warepublican wote wanahofia mashambulizi ya Orlando hayatokuwa ya mauaji ya mwisho ya watu wengi. Lakini kwa sasa hapo ndipo ushirikiano wa pande mbili unapomalizikia.
Labels:
Habari za Kisiasa
Location:
Washington, DC, USA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment