Wednesday, 22 June 2016

Dar: Mikononi mwa Polisi baada ya kutapeli akitumia jina la RC


JESHI la Polisi Mkoa Ilala linamshikilia mkazi wa Pugu, Imarock  Paula Rutashabya ‘ Issa Mohamed Jiunga’ kwa tuhuma za kutumia jina la mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa ajili ya kujipatia kipato kwa kupiga simu kwa watu wenye nafasi zao kwa kuomba fedha.

Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es  Salaam, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni amesema tukio hilo lilitokea Juni 16 mwaka huu maeneo ya mtaa wa Samora  Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.

Kamanda, Hamduni  amesema mtu alikamatwa baada ya kumpigia simu Mkurugenzi wa Kampuni ya Jones Logistics LTD , James Rodrick Luponda  na kujitambulisha kwa jina la Mkuu wa Mkoa wa Dar es  Salaam lengo la kumsaidia kijana wake aliyepata ufadhili wa kusoma lakini anahitaji achangie asilimia 30 sawa na dola za Kimarekani 35,000 ya gharama za chuo kilichoko nchini Ufilipino baada ya kupata ufadhili wa asilimia 70.

Amesema mtuhumiwa katika maongezi yake alimueleza mkurugenzi huyo kuwa fedha hizo atumie benki ya Eco akaunti Kenya au kutoa pesa taslim kwa  kumpa namba za simu 0717 338 473 ya kijana anayehitaji msaada kuwa atafika ofisini kwake baada masaa mawili akiwa na nyara zote za fursa ya hayo  masomo pamoja na akaunti namba ya benki alizozitaja.
Mtuhumiwa alikamatwa na anahojiwa  ili kuweza kupata mtandao wake ambao wanatumia majina ya viongozi kujipatia kipato.

Majina ya viongozi ambayo yanatumika kwa watu kujipatia kipato  kwa njia ya utapeli  ni Waziri Mkuu , Mkuu wa Mkoa na wengine na kuahidi wananchi kutoa ushirikiano dhidi ya watu wanaotumia majina hayo.

No comments:

Post a Comment